TANZANIA:_Maisha Plus East Africa 2016 Yazinduliwa kwa Kishindo


USIKU wa kuamkia leo ulikuwa na faraja kwa Watanzania na wafuatiliaji wa vipindi vya maisha halisi ambapo msimu mpya wa Maisha Plus East Africa 2016 ulizinduliwa rasmi katika Ofisi za Azam zilizopo Tabata jijini Dar.

Akizungumzia uzinduzi huo, Muanzilishi wa Maisha Plus, Masoud Kipanya alisema kuwa msimu huu mpya, Maisha Plus inakuja kivingine ikiwa na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu!

“Tunashukuru mwaka huu kwa mara ya kwanza tutaanza kuonekana katika TV ya Azam na kauli mbiu mwaka huu ni Hapa Kazi Tu, tumeona tutumie neno hilo kwa kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa lengo la kuhamasisha vijana wafanye kazi. Ni waambie tu Hapa Kazi Tu vijana watafurahi lakini wakiingia huko kambini itakuwa Hapa Tabu Tu,” alisema Masoud.

Maisha-Plus-7

Naye Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando alisema kuwa wamejipanga kutoa burudani ya tofauti.

“Tutakuwa na nchi kama Burundi, Rwanda na nyinginezo ambazo ni majirani zetu na zote hizo watatoa washiriki wanne kila moja hivyo kwa nchi za jirani tutakuwa na washiriki 16 na hapa Tanzania tutakuwa na washiriki 14 jumla watakuwa 30 ambapo Julai tutaanza rasmi.

“Ratiba itakuwa kuanzia Jumapili hii (Juni 5) ambapo kuanzia saa tatu usiku kupitia Azam Two tutaanza kurusha vipindi vya Maisha Plus vilipoanzia kwa kutumia teknolojia ya kisasa,” alisema Tido.

Baada ya uzinduzi huo, Maisha Plus itaanza safari za mikoni kuwapata washiriki kisha Julai wataingia rasmi kambini.

Maisha-Plus-17 (1) Maisha-Plus-14

Advertisements

Andika ngaho iciyumviro cawe ntutangwe

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s